We can help you tell the difference
between facts & fakes

Share
Comments

Chanjo ya Corona ni lazima kwa wanaosafiri kupitia Uwanja wa Ndege Dar?

Kuna taarifa nimeziona WhatsApp zinadai eti chanjo ni lazima kwa wasafiri. Ni kweli?

Last Updated on August 8, 2021 by Mexence Melo

Our narrated version of the story

Ni uongo, Wizara imetoa ufafanuzi

UFAFANUZI WA WIZARA YA AFYA: Hakuna sharti la chanjo ya Corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi. Ni vema msafiri akauliza Shirika la Ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea. Kwa nchi ambazo zinahitaji kipimo cha UVIKO-19, msafiri afanye kipimo hicho ndani ya masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari. Upimaji unafanyika kwa msafiri kufanya booking kupitia pimacovid.moh.go.tz ambapo atachagua kituo cha upimaji. Baada ya upimaji majibu yatatumwa kwake kwa njia ya barua pepe aliyotumia wakati wa booking. Akifika Airport cheti hicho kitahakikiwa katika dawati la afya. Unashauriwa kujiepusha na vyeti feki. Kuhusu uzushi unaoenea kwamba Chanjo ya UVIKO-19 inatolewa mashuleni hiyo sio kweli, Chanjo zote zinatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na Chanjo hiyo inatolewa kwa makundi Yale matatu yalivyotangazwa. Watoto sio walengwa wa Chanjo hii na vilevile hakuna kituo kwenye shule.
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Just In

View All

Fake

View All

Fact

View All

Welcome back

New to Jamii Check ?

File size limit: 20 mb

Post submited. Thank you !

Welcome to

Register

Already registered ?