Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni.
Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu.
Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Kuna dhana nyingi ambazo watu huishi wakiamini kuhusu hali ya ujauzito.
Dhana hizo hutofautiana kati ya jamii moja hadi nyingine.
Je, mdau wetu wa JamiiCheck unafahamu dhana zipi kuhusu hali ya ujauzito?
Zitaje upate undani wake
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje?
Je, kuna ukweli kwenye hili?
Wakuu,
Nimesikia sikia sehemu kuwa wakati wa tendo pale mwanaume akiwa anabana pumzi stamina inakua inaongezeka na anaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Kuna mwenye amewahi kushuhudia hili au kuna maelezo ya kisayansi yanayothibitisha hili? Mimi naona nilipigwa kamba tu hapa!
Kwenu wataalam wa JamiiCheck, ni ukweli au uzushi tu?
Kuna wazandiki huwa nawashangaa wanavyoponda pombe. Pombe haina madhara kama wanafiki wanavyotuaminisha. Pombe ni nzuri ukinywa kistaarabu, ina faida lukuki, ukibisha muulize Albert Chalamila.
Tafiti zinasema kuwa beer zinasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo. Kama mnavyojua magonjwa ya moyo yanaondoa watu kimya kimya hivyo mimi nawashauri tunywe beer kujilinda na magonjwa ya moyo.
Hata Biblia inasisitiza tunywe pombe tufurahie, na mkituona tunakunywa pombe msitukwaze.
Too much of anything is bad, but too much good whiskey is barely enough
Nimeona picha inasambaa mtandaoni ikimuonesha mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka ya kenya, Wafula Chebukati akiwa anaumwa, na maelezo mengine yanadai amesafirishwa kwenda Ujerumani kutibiwa.
JamiiCheck nisaidieni kuhakiki hii.
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa.
Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo.
Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.
Habari,
Nimeona tangazo Mtandaoni linadaiwa kutolewa na NEC, kwamba wametangaza nafasi za kazi ya uandishi wa daftari la kudumu la wapiga kura Mwaka 2024. Kinachonipa wasiwasi naona kama tovuti hii si rasmi.
Ukweli wake upoje?
Salaam,
Wakuu nimepata wenge baada ya kuona taarifa inaeleza watu 155 wamefafiki kwa Mafuriko Tanzania. Sijakutana na hii habari. Na hata Mtandao wa X (Twitter) wengine wanapata mashaka kama Mimi tu.
Je, kuna ukweli kwenye jambo hili?
Tunaombeni ufafanuzi
Habari JamiiCheck,
Mimi ni mjamzito, nimekuwa nasikia kuwa ulaji wa pilipili wakati wa Ujauzito kunafanya mtoto kuzaliwa na macho mekundu.
Nisaidieni kuhakiki hii maana napenda sana kula pilipili lakini naogopa mwanangu kuzaliwa na macho mekundu.
Kumekuwepo na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa makasha ya dawa za meno huwa na rangi (code) za aina mbalimbali zinazofafanua aina ya kemikali zilizotumika kutengenezea dawa hiyo.
Aidha, madai hayo yanafafanua zaidi kuwa kemikali husika ni hatari kwa afya na husababisha saratani, na kwamba makampuni yanayozalisha dawa hizi hayawezi kukupa siri hii.
Ukweli wake upoje?
Habari JamiiCheck,
Nimeona taarifa mtandaoni inayosema Pele ndiye mchezaji pekee duniani aliyeshinda Kombe la Dunia mara 3. Naona kama wanapotosha, inawezekana vipi asiwepo mchezaji mwingine zaidi yake?
Nimeona barua inasambaa Mtandaoni ikisema NECTA inaratibu zoezi la Kurekebisha Makosa ya majina kwenye vyeti vya Mwaka 2000-2023 kwa Malipo.
Barua hii inanipa mashaka sana, JamiiCheck nisaidieni kuhakiki.
Habari,
Ninanukuu kutoka kwenye meseji iiyotummwa kwenye kundi moja la Telegram ambalo mimi pia nimo.
Huku mitaani kuna taarifa kuwa kuwa uvunaji wa damu unaifanyika maeneo mbalimbali nchi huwa siku hizi hawatupi damu yoyote hata kama wataikuta ina ugonjwa wowote kwa kuwa damu hiyo wata muongezea mtu mwenye ugonjwa ulipo kwenye damu, mfano wakakuta damu waliyovuna ina virusi vya ukimwi hawaitupi akija mgonjwa mwenye ukimwi basi wata muongezea damu hiyo je hii ni kweli?
Inasadikika hili limechangiwa na ugumu wa kupata damu lakini pia hakuna shida yoyote mfano mtu ana virusi vya UKIMWI akiongezewa damu ya virusi vya UKIMWI kwa kuwa tatizo lake hapo ni damu si salama au isiyo salama, eti hata kama wangemuongezea damu iliyo salama bado...
Wakuu,
Nimekuja na swali hili baada ya jamaa mmoja kusema jambo hili sio la kweli, lakini mimi pia nimeshawahi sikia hii, bi mkubwa alituhadisia kuna ndugu yao mmoja aling'atwa na mbwa mwishowe alipokaribia kwenda kwenye ulimwengu mwingine alikuwa akibweka kama mbwa. Naamini hata wewe unayesoma hapa umeshawahi kusikia kuhusu hili.
Je, suala hili ni kweli au stori tu za mtaani wataalamu wa JamiiCheck?
Hii nimekutana nayo kwenye mitandao ya kijamii kuwa Serikali nchini Senegal inaachana na lugha ya Kifaransa ambayo ilikuwa lugha rasmi na sasa itatumia Kiarabu kama lugha rasmi ya shughuli za kiserikali.
Wakuu kuna ukweli wowote?
Hivi ni kweli kuwa ukomo wa kurefuka na kunenepa kwa uume ni miaka 20?
Yaani mtu mwanaume mwenye umri wa miaka 25 au 30, kamwe hawezi ku experience ongezeko la ukubwa wa uume wake?
Kwa maana nyingine, ukubwa wa uume wa mwanaume akiwa na miaka 20, ndio atakaokuwa nao akifikisha miaka 35?
Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo.
Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika.
Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.