JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni. Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu. Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Habari Jamiichek Kwa muda sasa katika Jamii yetu ya Kiswahili kumekuwa na hii nadharia kwamba mwanamke akitumia pombe Kali Aina ya konyagi au k vant halafu akaenda kufanya mapenzi, nitumie muda mrefu Sana kufika mshindo kitu ambacho inasemekana kinaearidhisha wanawake kiurahisi Huku mitaani, nimeshuhudia vijana wengi wakiingia katika mkumbo huu wa matumizi ya pombe Kali kwalengo wakashiriki mapenzi na wanawake zao na kuthibitisha uanaume wao, tena kulingana na wimbi kubwa la tatzo la upungufu wa nguvu za kiume imefanya pombe hizi kupendwa na vijana wengi zaidi Sasa ni vema Jamiichek na madaktari wa mambo ya uzazi hasa kwa wanaume mjitokeze mtoe ufafanuzi zaidi
Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri Mambo ya Ndani mwaka 1977 na Nafasi yake kuchukuliwa na Mzee Natepe. Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri Mzee Mwinyi kutoka katika nyumba ya Waziri arudi kwao Zanzibar ili yeye aweze kuishi hapo kama Waziri. Ilikuwa shida kidogo maana Mzee Mwinyi bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka. Nasikia Mzee Mwinyi ilibidi atoke hivyo hivyo bila kujiandaa lakini siku anatoka pale nyumbani alizuiwa na Mzee Natepe kuchukua mabati na mifuko ya simenti aliyokuwa amenunua kwa pesa zake mwenyewe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi. Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serikali. Kweli Mzee Mwinyi akaviacha akaondoka. Baada ya miaka kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa...
Wakuu, Msiniulize kwanini kuna picha ya mtu anakimbia wakati naongelea mambo ya tunda Nimesikia sikia sehemu kuwa wakati wa tendo pale mwanaume akiwa anabana pumzi stamina inakua inaongezeka na anaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi. Kuna mwenye amewahi kushuhudia hili au kuna maelezo ya kisayansi yanayothibitisha hili? Mimi naona nilipigwa kamba tu hapa! Kwenu wataalam wa JamiiCheck, ni ukweli au uzushi tu?
Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni: 1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa). 2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende. 3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake. 4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania. Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024. JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Wakuu, Nimekutana na taarifa imepostiwa na Times FM ikiwa na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu. Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza. Naomba kufahamu ukweli wa taarifa hii, maana nimependa sana haya maneno nataka niitumie sehemu.
Katika mitandao ya kijamii nimeona video inayohusishwa na Rais Mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, akikemea Ufaransa kuwa ni wakati wa kuondoka bara la Afrika. Video hiyo inamuonesha Rais Faye akiimbia Ufaransa kuwa "Inakuwa wakati wa Ufaransa kuinua magoti yake kutoka shingoni mwetu na kumaliza ukandamizaji huu usio wa haki. Karne nyingi za mateso, biashara ya binadamu, ukoloni, na ukoloni mamboleo vimesababisha mateso yasiyohesabika. Ni wakati wa kumaliza mzunguko huu wa ukandamizaji," Wachangiaji wengi kwenye video hizo zinazozunguka mitandaoni walionesha furaha kwamba Rais Faye ameonesha msimamo imara dhidi ya Ufaransa kulikandamiza bara la Afrika. Video hiyo inanipa mashaka.
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Back
Top Bottom