JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

JamiiCheck ni Moja kati ya Majukwaa yanayopatikana ndani ya tovuti ya JamiiForums.com. Jukwaa hili limewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki, kutafuta uthibitisho au uhalisia wa habari, taarifa, matukio, picha au video mbalimbali zinazojitokeza au kuibuka kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya mtandao. Tofauti na Majukwaa na vyombo vingine vya kuhakiki ukweli wa habari, JamiiCheck ni Jukwaa pekee linalotoa fursa kwa watumiaji wake (Wanachama wa JamiiForums.com) kushiriki katika uhakiki kwa kuleta taarifa, picha au Video mbalimbali ambazo wanahitaji kuzichunguza kupata ukweli au chanzo chake pamoja na kuchangia/ kutoa maoni kwenye taarifa nyingine zilizohakikiwa. Ikiwa utakutana na habari au taarifa yoyote inayokutatiza...
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni. Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu. Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
Salaam Wakuu, Nimekutana na stori mtaani zinadai kwamba mnamo mwaka 1990 Bondia Maarufu Muhamedi Ali alienda nchini Iraq kuzungumza na rais wa nchi hiyo wakati huo Sadam Hussein kuwaachia mateka wa Marekani na kufanikiwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu sakata hili? Tunaombeni ufafanuzi ====== Muhammad Ali alizaliwa mnamo 17 Januari 1942 na alifariki 3 Juni 2016. Muhammad Ali alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975 Ndipo alipobadili jina na kuanza kufahamika kama Muhammad Ali. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara...
Wakati wa Uchaguzi baadhi ya Watu huibuka na kutengeneza akaunti 'feki' na kuzipa majina ya Wagombea au kubadili jina la akaunti zao na kutumia jina la mgombea fulani. Akaunti hizo hutumika kutengeneza taarifa au maudhui mbalimbali yanayomuhusu Mgombea wa Uchaguzi, hutumika kupotosha taarifa, kuchafua Wagombea wengine au kuharibu taswira ya Mgombea kwenye Uchaguzi husika. Hivyo, ni muhimu kufanya uhakiki wa kila akaunti inayotengeneza maudhui au kutoa taarifa wakati wa Uchaguzi ili kuepuka kupotoshwa. Kubaini akaunti feki za mitandao ya kijamii zinazotumia jina la mgombea wakati wa uchaguzi inaweza kuwa changamoto, lakini kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kufanya hivyo: Angalia Uhakika wa Akaunti: Mara nyingi, mitandao ya kijamii...
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akiwa katika Mkutano wa Tatu wa Demokrasia uliofanyika Machi 18, 2024 ametoa wito kwa viongozi wote Ulimwenguni kuunga mkono jitihada za kukomesha taarifa potofu Yoon ameeleza Taarifa zisizo za kweli wakati wa Uchaguzi huweza kuathiri mchakato mzima wa Demokrasia kwa kuwafanya Wananchi wafanye maamuzi yasiyo sahihi yanayotokana na taarifa zisizo na ukweli Korea Kusini inatarajiwa kuwa na Uchaguzi hivi karibuni huku ikidaiwa Nchi hiyo imekumbwa na tabia ya kusambaa kwa taarifa nyingi potofu kupitia Mitandao ya Kijamii.
Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni: 1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa). 2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende. 3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake. 4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta sigara ambapo 80% kati yake wanatoka kwenye nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati. Aidha, takriban watu Milioni 7 hupoteza maisha kutokana na athari za moshi wa sigara unaotokana na kuvuta sigara moja kwa moja au pia kuvuta moshi uliotolewa na mvutaji wa Sigara. Tumbaku huathiri karibu kila kiungo na mfumo katika mwili, ikisababisha matatizo mbalimbali kama vile saratani, Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Ugonjwa wa Mishipa ya Moyo, Kiharusi...
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania. Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024. JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Pamoja na ukweli kuwa teknolojia imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya habari na mawasiliano, ambapo sasa mtu yeyote(Netizen) anaweza kutoa taarifa ikawafikia watu wengi kwa haraka sana, lakini ni vyema kuhakiki na kuthibitisha taarifa yoyote ambayo unaona inaweza kuzua taharuki kabla hujaiweka mtandaoni Pindi itokeapo ajali, wananchi wamekuwa wakisaidia kwa nia njema kusambaza taarifa za ajali hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Kasoro hutokea pale wanapotoa taarifa za vifo ambazo zinakuwa bado hajizathibitishwa na mamlaka husika. Unakuta kuna ajali ya basi imetokea, mwananchi aliyejitolea kusambaza taarifa hizo, bila kuwa na uelewa anaweza kupotosha kwa kutaja idadi ya vifo isiyo sahihi mfano kwa kusema watu wote waliopata ajali...
Kuna picha nimeona Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama akizindua uidhinishaji wake wa mwisho wa mgombea urais 2022 nchini Kenya ambapo alionesha wazi kumuunga mkono Naibu Rais Ndugu William Ruto. Barack Obama ana vinasaba vya Ujaluo, sijui ilikuwa vipi akashindwa kumuunga mkono Mjaluo mwenzio Mwamba Raila Amolo Odinga. Chanzo: BBC === Video halisi iliyotumika kutengeneza picha hiyo
Wakati wa uchaguzi, baadhi ya watu hutengeneza taarifa za uongo au kuficha ukweli kuhusu historia ya mgombea fulani ili kuathiri taswira yake kwa umma. Taarifa hizo zinaweza kuwa mwaka wa kuzaliwa, historia ya uraia wake, au elimu yake. Mathalani, mtu au kundi la watu linaweza kusambaza taarifa za uwongo kuhusu umri wa mgombea kuonesha kama ni mdogo au mkongwe zaidi kuliko uhalisia, ikitegemea jinsi umri unavyoweza kuathiri jinsi watu wanavyomwona mgombea. Vilevile, historia ya uraia au elimu ya mgombea inaweza kupotoshwa ili kujenga mazingira ya kumsafisha au kumharibia katika uchaguzi husika. Mfano, kwenye uchaguzi wa Marekani mwaka 2018 historia ya Barack Obama ilipotoshwa kwa watu kumzushia kuwa asili ya Obama ni Kenya taarifa...
Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza kuchubua utumbo. Sasa hii ya kuambukiza kwangu imekuwa mpya sana, tena mwandishi alifafanua zaidi kuwa eti iwapo mwenza wako ana ulcers basi uwezekano wa wewe kuupata ni mkubwa maana anaweza kukuambukiza.
Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo. Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika. Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...
Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri Mambo ya Ndani mwaka 1977 na Nafasi yake kuchukuliwa na Mzee Natepe. Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri Mzee Mwinyi kutoka katika nyumba ya Waziri arudi kwao Zanzibar ili yeye aweze kuishi hapo kama Waziri. Ilikuwa shida kidogo maana Mzee Mwinyi bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka. Nasikia Mzee Mwinyi ilibidi atoke hivyo hivyo bila kujiandaa lakini siku anatoka pale nyumbani alizuiwa na Mzee Natepe kuchukua mabati na mifuko ya simenti aliyokuwa amenunua kwa pesa zake mwenyewe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi. Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serikali. Kweli Mzee Mwinyi akaviacha akaondoka. Baada ya miaka kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa...
Shirika la habari la AFP wakiwa wanatoa mafunzo mtandaoni wamebainisha namna upotoshaji wakati wa Uchaguzi unaweza kutokea kwa Mgombea, Chama pamoja na Mfumo. Wanaeleza, Upotoshaji kwa Mgombea hulenga kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu Mgombea fulani. Upotoshaji wa Chama cha Siasa hukusudia kutoa taarifa za uongo kuhusu chama fulani cha siasa kinachoshiriki uchaguzi. Aidha, Upotoshaji unaohusu mfumo wa Uchaguzi hulenga kutoa taarifa za uongo zinazoathiri zoezi la upigaji kura na utangazi matokeo ya Uchaguzi. Aina zote hizo za upotoshaji hulenga kuharibu au kutengeneza upande fulani wa chama cha Siasa ili kiweze kunufaika au kuathirika na Uchaguzi unaoendelea
Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha 1. Tembelea Google Image Search Fungua kivinjari chako na nenda kwenye ukurasa wa Google. Bonyeza kwenye sehemu ya 'Images' au 'Picha' kwenye ukurasa wa kwanza wa Google, au ingiza 'Google Image Search' moja kwa moja kwenye sanduku la utafutaji wa Kifaa chako 2. Ingiza Picha Kuna njia kadhaa za kuingiza picha kwenye Google Image Search: Bonyeza kitufe cha kamera kilichopo kwenye sanduku la utafutaji ili kuwezesha utafutaji wa picha kwa kutumia kamera. Kama picha unayo kwenye kifaa chako, unaweza kuiweka moja...
Back
Top Bottom